Upeo wa Mapenzi

Nimefika upeo wa furaha!

Fikira zangu kwako kanipa karaha. 

Nilipokutizama mwili wangu wote ulizama.

Kanipa nguvu kufika kilele,

Ukaninyanyua nitembe.

Kinywa kimya bila tenzi,

Dumbala kunitoka bila aibu.

Nasfi yangu kachezacheza ulipotabasamu lazizi,

Huku pumzi kunipunguka.

Uzuri wako ulifanya nilie kishenzi.

Eh! nitapagawa au niwe chizi wa mapenzi!

Uumbaji huu sikuona kasoro,

Ila nilijua hakuna aliyekamilika.

Kama asali nilitamani kukuonja onja,

Kukugusa ngozi lako la strungi taratibu

Na kukumbatia siku zote. 

Penzi langu kwako umenishinda uzito,

Sasa nakupa ya ziada, naomba uipoke.

Niliomba Mungu nimpate kama wewe,

Ukamilishe uzima wangu

Amani wa moyo wangu.

Naamini tutapaa pendoni!

Vitendo vyetu vikiambatana kwa umoja. 

Kukupenda si tazizi,

Nami naapa kukupa thamani ya mapenzi yanayokufaa.

Kama sio wewe, nani atayenimiliki?

Chante_ze_weirdo™ ©2017

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s